Nini dhambi kwa mwenye dhiki?
4
views
Lyrics
All my people East Africa Tanzania, Uganda and Kenya Dar es Salaam, A town Wherever you are Piga magoti, tuombe Mungu Hii ni siasa, dini, vita, ubwana, utwana, au kiama ghalika, sodoma na gomora? Simama imara, zunguka kila kona, kila anga angaza Kushoto, kulia, mbele, nyuma kote pitia Na hapo ulipojishikiza g'ang'ania, sikilizia, vumilia baadae usije jutia Hii ni mahususi na maalum kwa watu wangu Walemavu, vipofu, zeruzeru na wendawazimu Watoto wa mitaani, fukara, masikini na wenye akili zao timamu Hii kamba ngumu Mjue tunavutana na wenye nguvu Vitambi na mashavu Hakuna tena fair game Refarii kauzu Uwanja wenyewe mkavu Ujira mgumu, malipo finyu Kilichobaki kucheza rafu Tumechoshwa na ukabaila, ubepari na ubeberu Wakati ndo huu Ukombozi ndo huu Na sasa naamuru mliopo chini wote mpate divai ya vinibu Mtetezi wenu nikaze gidamu Nimwage sumu ya ----- juu yao Wajikune bila aibu Kwanza saluti kwa waliyotangulia kuzimu Pili tuombe Mungu Baba yetu, utupe mkate wetu wa kila siku Utujaze nguvu Tupate kudumu ndani ya game Tutakapofika kuzimu siku ya hukumu Utupe nafasi tupate kutubu Kwani tunajua tunatenda maovu Tunakula haramu Tunatumia kila mbinu Juju, uhalifu, upanganyifu Ili tuweze kujikimu Lakini isiwe kisingizio kwa wanadamu wengine kunyimwa haki zetu Kutuzibia riziki zetu Kutuita makafiri, dharau na kutukashifu Kwani nini dhambi Nini dhambi kwa mwenye dhiki, Kipi haram, kipi halali, Kila mmoja anaitaka hii riziki Kitendawili, vurugu mechi Huwezi tabiri Kwa nini? Uliza swali, kama sote tungekuwa wasomi, matajiri Ni nani angelifanya kazi za kutisha na hatari mfano ya mochwari Kila mmoja wetu hapa mjini kaja kwa dili Kila kitu, kila mahali Na hata ngozi ya mtu dili Wengine wachawi, waganga feki Matapeli, wasafiri ------ Wakati wengine wapole kama walokole Mchana pirika nyingi maofisini Kumbe night kali, kahaba Shuga, jambazi, mengine ya kusitiri Ah! Wapo waliopoteza maisha katika kufight life Kumbukumbu zao zimebaki makaburini Na wapo waliopoteza kabisa tumaini la kuwini Hao roho zao utadhani wamezitoa rehani Wakikutight mahali fulani Inabidi uwakabidhi mshahara wote wa mwisho wa mwezi () Kweli Bongo kutafuta braza Utajajuta utakapojikuta huna hata bukta Shauri yako we tegesha tu kama golikipa Na hao unaowategemea mwishowe watakutosa Huna elimu, hun fani Lakini nguvu, hulimi, uchumi unao unaukalia Kumbuka Kupata au kukosa yote ni kawaida Sometimes unalala unaota unakula Unakunywa, unapiga denda Na kula uroda na demu bomba Ukikurupuka tu unakuta patupu Hakuna kitu (, Yamat singing a traditional Maasai song)
Audio Features
Song Details
- Duration
- 04:37
- Key
- 5
- Tempo
- 90 BPM